Deuteronomy 1:26-31

26 aLakini hamkuwa tayari kukwea, mkaasi dhidi ya amri ya Bwana Mwenyezi Mungu wenu. 27 bMkanung’unika ndani ya mahema yenu na kusema, “Bwana anatuchukia, kwa hiyo alitutoa Misri ili kututia mikononi mwa Waamori kutuangamiza. 28 cTwende wapi? Ndugu zetu wametufanya kufa moyo. Wanasema, ‘Watu wa huko wana nguvu zaidi na ni warefu kuliko sisi tulivyo; miji ni mikubwa, yenye kuta zilizofika juu angani. Zaidi ya hayo, tumewaona Waanaki huko.’ ”

29 dNdipo nikawaambia, “Msihofu, wala msiwaogope. 30 e Bwana Mwenyezi Mungu wenu anayewatangulia, atawapigania, kama alivyofanya kwa ajili yenu huko Misri, mbele ya macho yenu hasa, 31 fna pia huko jangwani. Huko mliona jinsi Bwana Mwenyezi Mungu wenu alivyowachukua, kama baba amchukuavyo mwanawe, katika njia yote mliyoiendea mpaka mkafika mahali hapa.”

Copyright information for SwhKC